Kukodisha wanawake kuja kucheza dufu kwenye harusi

Swali: Je, ni jambo limewekwa katika Shari´ah wanawake kucheza dufu katika harusi, je, inajuzu vilevile kukodisha wanawake kwa ajili ya hilo?

Jibu: Ndio, inajuzu. Kitendo hichi si kwamba kinajuzu tu bali kimewekwa vilevile katika Shari´ah. Inajuzu kuchukua ujira kwa vitu ambavyo vimewekwa katika Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Allaah akiharamisha kitu, basi anaharamisha vilevile thamani yake.”

Chukua kanuni mbili kutoka kwenye Hadiyth hii:

1- Akiharamisha kitu, Anaharamisha vilevile thamani yake.

2- Akihalalisha kitu, Anahalalisha vilevile thamani yake.

Pamoja na kwamba inajuzu kuajiri mwanamke mwenye kucheza dufu. Hata hivyo thamani lazima iwe mantiki. Kupewa 1,523 $ kwa sababu ya kucheza saa moja au mbili tu si sahihi. Ni kupetuka mipaka na israfu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (11)
  • Imechapishwa: 21/09/2020