Swali: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameniruzuku watoto wawili. Kila mtoto mmoja amezaliwa na vidole ishirini na nne ziada. Unasemaje iwapo nitavikata kwa daktari?

Jibu: Wanachuoni wametaja kuhusiana na masuala haya kwamba haijuzu kukata vidole vya ziada. Kilicho dhahiri ni kwamba haijuzu kufanya hivo kutokana na ile khatari kwa yule mwenye vidole hivyo. Kwa wakati wa sasa khatari ni ndogo na madhara yako mbali. Kile ambacho tunaona ni kwamba hakuna neno kukata vidole vilivyozidi vinavyoonekana vibaya kimaumbile. Ama vidole vikiwa vimezidi lakini hata hivyo havileti muonekano mbaya kinachotakikana vibaki vilivyo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (12) http://binothaimeen.net/content/6759
  • Imechapishwa: 11/12/2020