Kinachotarajiwa kwa wanafunzi wanaotakharuji

Chuo kikuu hiki kimejikita katika masomo maalum. Kimejikita katika kuilinda ´Aqiydah sahihi, ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Nyinyi ni warithi wa waliokutangulieni. Baada yao nyinyi ndio ambao mtasimamia kuilinda ´Aqiydah hii. Haihusiani na kulinda ´Aqiydah ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, bali ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao ni wale Maswahabah, wanafunzi wa Maswahabah na wale waliowafuata kwa wema.

Hawezi kuitetea ´Aqiydah hii isipokuwa yule mtu ambaye ameifahamu na akaielewa. Nyinyi mnafanya kazi muhimu pindi mnaposoma, mkafundisha na kulingania katika dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/14-05-1437.mp3 Muhadhara: Himaayat-ush-Shabaab min-al-Afkaar al-Haddaamah
  • Imechapishwa: 11/12/2020