Swali: Ni ipi hukumu ya kurekodi mihadhara ya video misikitini?

Jibu: Hapana shaka kwamba picha hazina kheri yoyote. Lakini ikiwa lengo ni jema na sio kwa sababu yule mzungumzaji apate kuwa maarufu au kuonyesha kuwa amefanya muhadhara mbele ya mkusanyiko mkubwa wa watu, bali anachotaka ni kubainisha kuwa mkusanyiko mkubwa huu wa watu wamekuja kusikiliza kheri na mawaidha, nataraji kuwa ni sawa. Vinginevyo hakuna haja ya kuchukua video. Ni vyema na uzuri ulioje ikiwa hakuna picha yoyote inayoingizwa misikitini?

  • Mhusika: ´Allâmah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Haqiyqat-ul-Bay´ah fiyl-Islaam wa Bayaan Shuruutwihaa wa Khatwar Naz´ihaa http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=148858
  • Imechapishwa: 11/12/2020