Kukaa na imamu katika Tashahhud au swalah nyingine ya mkusanyiko?

Swali: Mtu ameingia msikitini na akamkuta imamu ameketi chini katika Tahiyyaat katika Rak´ah ya mwisho ambapo akajiunga naye na kuketi chini. Wakati aliposimama kukidhi Rak´ah zilizompita akawasikia watu wanaswali. Je, akate swalah yake hii na ajiunge pamoja na swalah ya mkusanyiko?

Jibu: Ni mwenye kupewa khiyari; akitaka ataitaka na kujiunga pamoja nao kwa ajili ya manufaa ya kuswali na mkusanyiko na akitaka atakamilisha.

Swali: Ni kipi bora?

Jibu: Ni vizuri akiikata au akageuza nia kuwa ni swalah inayopendeza kisha akaenda kuswali pamoja nao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22326/هل-التشهد-مع-الامام-افضل-ام-جماعة-اخرى
  • Imechapishwa: 05/02/2023