Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kujirejea funga yake iliyopendekezwa au ya deni kabla ya kupambazuka alfajiri?
Jibu: Hapana kuzuizi kwa mtu kujirejea funga yake kwa sababu hajaanza swawm yake. Kwa sababu akifungika nia na akafunga basi itamlazimu kukamilisha siku hii na haitojuzu kwake kuikata. Wanazuoni wamesema:
“Ambaye ataingia ndani ya faradhi iliyopanuliwa basi ni haramu kwake kuikata.”
Swali: Hata kama itakuwa swawm ya wajibu kama vile swawm ya nadhiri au ya kafara?
Jibu: Kila swawm ambayo ni ya lazima – ni mamoja ya kulipa deni, nadhiri au kafara – mtu akishaingia ndani yake na akaanza kufunga siku yake, basi atalazimika kuikamilisha na wala haitojuzu kwake kuikata isipokuwa kutokana na udhuru wa kilazima.
Swali: Akiikata nia hukumu yake inakuwa kama hukumu ya kafara ya Ramadhaan?
Jibu: Hukumu yake haiwi kama hukumu ya kula katika Ramadhaan. Lakini hata hivyo anapata dhambi kwa kitendo hicho.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/392)
- Imechapishwa: 26/03/2022
Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kujirejea funga yake iliyopendekezwa au ya deni kabla ya kupambazuka alfajiri?
Jibu: Hapana kuzuizi kwa mtu kujirejea funga yake kwa sababu hajaanza swawm yake. Kwa sababu akifungika nia na akafunga basi itamlazimu kukamilisha siku hii na haitojuzu kwake kuikata. Wanazuoni wamesema:
“Ambaye ataingia ndani ya faradhi iliyopanuliwa basi ni haramu kwake kuikata.”
Swali: Hata kama itakuwa swawm ya wajibu kama vile swawm ya nadhiri au ya kafara?
Jibu: Kila swawm ambayo ni ya lazima – ni mamoja ya kulipa deni, nadhiri au kafara – mtu akishaingia ndani yake na akaanza kufunga siku yake, basi atalazimika kuikamilisha na wala haitojuzu kwake kuikata isipokuwa kutokana na udhuru wa kilazima.
Swali: Akiikata nia hukumu yake inakuwa kama hukumu ya kafara ya Ramadhaan?
Jibu: Hukumu yake haiwi kama hukumu ya kula katika Ramadhaan. Lakini hata hivyo anapata dhambi kwa kitendo hicho.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/392)
Imechapishwa: 26/03/2022
https://firqatunnajia.com/kujirejea-nia-kabla-ya-kupambazuka-alfajiri/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)