36. Amekata swawm kwa adhaana iliotolewa kabla ya wakati

Swali: Muadhini aliadhini ambapo tukakata swawm zetu. Baadaye ikatubainikia kuwa ameadhini dakika kadhaa kabla ya kuingia wakati. Ni kipi kinachotulazimu na ni kipi unachowanasihi waadhini?

Jibu: Ni lazima kwenu muilipe siku hiyo. Nawanasihi ndugu zangu waadhini wamche Allaah juu ya nafsi zao. Wanapasa kujua kuwa ni wenye kuaminiwa juu ya nyakati, swalah na funga za waislamu. Kwa hiyo wasiadhini kabla ya kuingia wakati. Kwa sababu jambo hili linasababisha kuharibika kwa swawm kwa yule atakayefungua. Pengine vilevile ikapelekea kuharibika kwa swalah kwa yule ambaye ataswali papo hapo baada ya adhaana. Hivyo basi, ni lazima kwao kumcha Allaah na wasiziharibu funga na swalah za watu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 24/03/2022