Kujirejea nia kabla ya kupambazuka alfajiri

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kujirejea funga yake iliyopendekezwa au ya deni kabla ya kupambazuka alfajiri?

Jibu: Hapana kuzuizi kwa mtu kujirejea funga yake kwa sababu hajaanza swawm yake. Kwa sababu akifungika nia na akafunga basi itamlazimu kukamilisha siku hii na haitojuzu kwake kuikata. Wanazuoni wamesema:

“Ambaye ataingia ndani ya faradhi iliyopanuliwa basi ni haramu kwake kuikata.”

Swali: Hata kama itakuwa swawm ya wajibu kama vile swawm ya nadhiri au ya kafara?

Jibu: Kila swawm ambayo ni ya lazima – ni mamoja ya kulipa deni, nadhiri au kafara – mtu akishaingia ndani yake na akaanza kufunga siku yake, basi atalazimika kuikamilisha na wala haitojuzu kwake kuikata isipokuwa kutokana na udhuru wa kilazima.

Swali: Akiikata nia hukumu yake inakuwa kama hukumu ya kafara ya Ramadhaan?

Jibu: Hukumu yake haiwi kama hukumu ya kula katika Ramadhaan. Lakini hata hivyo anapata dhambi kwa kitendo hicho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/392)
  • Imechapishwa: 26/03/2022