Swali: Ni kipi bora zaidi kati ya kujifunza elimu au kupigana jihaad katika njia ya Allaah?

Jibu: Kujifunza elimu ni katika kupigana jihaad katika njia ya Allaah. Atafute elimu kwanza ndio apambane jihaad. Ni lazima kwake aielewe dini kwanza. Isipokuwa ikimuwajibikia jihaad na ikawa ni faradhi kwa kila mmoja. Hapo ni pale ambapo adui atashambulia au zikahudhuria safu mbili. Katika hali hii ni lazima kwake kupambana jihaad. Lakini muda wa kuwa bado yuko na nafasi basi ni lazima kwake kuisoma na kujifunza dini ili ajue namna atakavyopambana jihaad.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21708/ايهما-افضل-طلب-العلم-او-الجهاد-في-سبيل-الله
  • Imechapishwa: 23/09/2022