Swali: Mtu akiwalingania wazazi wake kuacha baadhi ya maasi na wasiitikie inafaa kwake kuondoka nyumbani na kuwaacha?

Jibu: Hapana, awatendee wema. Allaah amesema kuhusu wazazi makafiri:

وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ

“Hata hivyo suhubiana nao kwa wema duniani na ifuate njia ya anayerudi Kwangu.” (31:15)

Hata wazazi makafiri mtu anatakiwa kuwafanyia upole na wema na kuwaangalia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21707/كيف-يكون-البر-بالوالدين-العاصيين
  • Imechapishwa: 23/09/2022