Swali: Je, inafaa kuswali huku mtu ameweka kitambaa puani au mdomoni au kutegemea ukuta au nguzo na mfano wake?

Jibu: Imechukizwa kuswali huku mtu amejifunga kitambaa puani au mdomoni isipokuwa kukiwepo kuna sababu. Haijuzu katika swalah ya faradhi kutegemea ukuta au nguzo. Kwa sababu ni lazima kwa anayeweza kusimama kwa kunyooka pasi na kutegemea kitu. Kuhusu swalah ya sunnah hapana vibaya. Kwa sababu inafaa kuiswali kwa kuketi. Kuiswali kwa kusimama ni bora zaidi kuliko kukaa chini.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/114)
  • Imechapishwa: 16/10/2021