Anayeswali peke yake kusoma kwa sauti ya juu

Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma kwa sauti ya juu kwa ambaye anaswali peke yake? Je, inafaa akasoma kimyakimya?

Jibu: Kusoma kwa sauti ya juu, kama katika Fajr, Maghrib na ´Ishaa kwenye Rak´ah ya kwanza na ya pili imependeza kwa imamu na anayeswali peke yake. Atakayesoma kimyakimya hapana vibaya kwake. Lakini ameacha Sunnah. Anayeswali peke yake akiona kuwa kusoma kimyakimya ndio kunamfanya kuwa na unyenyekevu basi hapana neno kwake. Imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alikuwa katika swalah ya usiku mara akisoma kwa sauti ya juu na mara akisoma kimyakimya. Hayo yametajwa na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kuhusu imamu imependekeza kwake siku zote kusoma kwa sauti ya juu kwa ajili ya kumwigiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Faida nyingine ni yeye kuwanufaisha maamuma kuwasikilizisha maneno ya Allaah (Subhaanah) ni mamoja katika swalah ya faradhi au ya sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/116)
  • Imechapishwa: 16/10/2021