Swali: Ni ipi hukumu ya kucheza na ndevu au nguo wakati wa swalah?

Jibu: Haijuzu kucheza na ndevu au nguo katika swalah. Bali ni lazima kutulia. Allaah (Ta´ala) amesema:

قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ

“Hakika wamefaulu waumini; ambao katika swalah zao ni wenye kunyenyekea.”[1]

Kilichowekwa katika Shari´ah kwa muislamu ni yeye awe na unyenyekevu katika swalah yake na asicheze si na ndevu zake wala nguo yake. Lakini kitu kidogo kinasamehewa na kingi hakijuzu.

[1] 23:01-02

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/110)
  • Imechapishwa: 16/10/2021