Kujenga nyumba juu ya msikiti

Swali: Kuna mtu amejitolea ardhi na akakusanya pesa ili kujengwe msikiti.  Baada ya msikiti kukamilika akajenga juu ya msikiti nyumba. Je, inafaa kwake kufanya hivo?

Jibu: Ikiwa alinuia hilo tangu mwanzo. Hapana vibaya ikiwa alinuia tangu mwanzo kujenga nyumba na chini yake kuweka msikiti. Lakini ikiwa hakunuia hivo tangu mwanzo bali ni jambo limejitokea baadaye haifai kwake kujenga makazi juu ya msikiti. Ikiwa aliwaeleza tangu mwanzo. Ama ikiwa hakuwaeleza tangu mwanzo asijenge juu yake kitu. Sehemu yote ya juu ni katika msikiti. Lakini wamekubaliana na kamati ya msikiti kuweka makazi yake juu yake, hapana vibaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23641/حكم-بناء-منزل-فوق-المسجد
  • Imechapishwa: 07/03/2024