Swali: Katika mji wetu kuna ada ilioenea ya dhambi kubwa ambayo ni kutukana dhati ya Allaah. Ni ipi hukumu ya Uislamu kwa hili? Je, mke mwenye kufanya hivi atalikiwe ilihali hakubali hili?

Jibu: Kutukana dhati ya Allaah ni dhambi kubwa kabisa, bali ni kuritadi kutoka katika Uislamu. Ni wajibu kwa mwenye kutumbukia katika hilo akimbilie kuleta tawbah na msamaha. Vilevile akithirishe kufanya matendo mema. Akitubu tawbah ya kweli Allaah atamsamehe na mke wake atakuwa katika ulinzi wake kwa kutubia kwake.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/11)
  • Imechapishwa: 24/08/2020