Baadhi ya mambo yenye kumtoa mtu katika Uislamu

Swali: Ninakuomba unitajie hali zote ambazo zinamkufurisha mtu na kumtoa katika Uislamu na hukumu ya kafiri huyu, kuritadi, kufuru ndogo, kupenda kwa ajili ya Allaah na kuchukia makafiri kwa ajili ya Allaah.

JIbu: Mambo yenye kukufurisha ambayo yanamtoa mtu katika Uislamu ni mengi. Miongoni mwayo ni kukanusha kitu ambacho kinajulikana fika kuwepo kwake katika Uislamu. Katika mambo hayo ni kama kukanusha uwajibu wa swalah, zakaah, swawm, hajj na mfano wake. Vilevile kuhalalisha kitu ambacho kinajulikana fika uharamu wake katika Uislamu. Katika mambo hayo ni kama zinaa, kunywa pombe, kuua nafsi kwa kukusudia pasi na haki, kuwaasi wazazi wawili na mfano wa hayo. Miongoni mwa mambo hayo pia kunaingia kumtukana Allaah, Mtume Wake, Uislamu, Malaika na mfano wa hayo. Kuhusu kwa kina zaidi rejea katika milango yenye kuzungumzia hukumu ya mwenye kuritadi katika vitabu vya Fiqh ili uweze kujua.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/11-12)
  • Imechapishwa: 24/08/2020