Swali: Je, inajuzu kwetu kuamini kufuru ya wanawake waliovaa lakini bado wako uchi kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hawatoingia Peponi na wala hawatonusa harufu yake… ”?

Jibu: Ambaye ataamini kuwa ni halali katika wao anakufuru baada ya kubainishiwa na kumjuza hukumu. Asiyehalalisha hilo katika wao, lakini akatoka amevaa lakini bado yuko uchi, sio kafiri. Lakini hata hivyo amefanya dhambi kubwa. Ni wajibu kujivua nayo na kutubia kwayo kwa Allaah. Huenda Allaah akamsamehe. Akifa juu ya dhambi hiyo kabla ya kutubia yuko chini ya matakwa ya Allaah kama watenda madhambi wengine wote. Allaah (´Azza wa Jall) anasema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakaye.” (04:116)

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/16)
  • Imechapishwa: 24/08/2020