Swali: Naishi na watu ambao baadhi yao hawaswali na wengine wanaswali kwa kuchelewa ambapo wanaswali Fajr saa tatu pamoja na kuzingatia kuwa tunafanya kazi katika kampuni moja. Je, niache kazi hii?

Jibu: Mosi wanasihi marafiki zako, wakhofishe juu ya Allaah, wapendezee kheri, watahadharishe kupuuza swala, waamrishe nayo na kuihifadhi kwa nyakati zake msikitini. Ikiwa huna mawasiliano nao isipokuwa kazini peke yake basi jitenge nao. Isipokuwa utangamane nao kwa kutaraji utawanasihi na watakubali nasaha kutoka kwao. Vinginevyo ikiwa hakuna kitu kingine kinachowafungamanisha zaidi ya kazi, basi jitenge nao muda wa kuwa ni wenye kuzipoteza, wanahisi uvivu na kupuuza swalah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-السكن-مع-من-يتهاون-بالصلوات-وخصوصاً-صلاة-الفجر
  • Imechapishwa: 11/06/2022