54. Nguzo ya tano: Kuinuka kutoka katika Rukuu´


Maneno yake:

“… kuinuka kutoka kwenye Rukuu´.”

Nguzo ya tano miongoni mwa nguzo za swalah ni kuinuka kutoka kwenye Rukuu´. Kuinua kichwa kutoka katika Rukuu´. Hili ni kwa mujibu wa madhehebu ya Hanaabilah na wanazuoni wengi[1].

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika Rukuu´ na vivyo hivyo kutoka katika Sujuud basi husimama akanyooka barabara mpaka akasema mwenye kusema:

“Amesahau.”[2]

[1] Tazama ”al-Majmuu´” (03/377).

[2] al-Bukhaariy (821) na Muslim (742).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 87
  • Imechapishwa: 21/06/2022