Swali: Baada ya kumaliza kutawadha niliingiwa na mashaka kama nilifuta juu ya soksi au hapana. Hata hivyo sikurudi kutawadha tena na nikaswali. Je, kitendo changu hichi ni sahihi?

Jibu: Mashaka baada ya kumaliza ´ibaadah hayadhuru. Lakini ukiingiwa na mashaka mwanzoni mwa ´ibaadah basi unatakiwa kushika lililo salama. Ikiwa ni katikati ya wudhuu´, basi unatakiwa kukamilisha kile ulichokitilia mashaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (50) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah%20Fiqh-06-05-1437.mp3
  • Imechapishwa: 17/03/2019