Kuharakisha eda kwa kutumia dawa ya kuleta hedhi

Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia dawa ya kuleta hedhi kwa kuzingatia ya kwamba mwanamke huyo yuko ndani ya eda ya talaka rejea?

Jibu: Hapana. Asitumie kwa ajili ya kuharakisha eda iishe. Asifanye hivyo. Ama kutumia kwa ajili ya maradhi baada ya kupata ushauri kutoka kwa daktari, ni sawa. Lakini ni mwenye afya na yuko salama, anatumia kwa ajili ya kuharakisha eda, hapana. Haijuzu kufanya hivyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ls–14330811.mp3
  • Imechapishwa: 06/10/2020