Swali: Mtu akigusa dhakari yake wakati wa kuoga josho la janaba. Je, unachenguka wudhuu´ wake?
Jibu: Maoni yanayotambulika katika madhehebu ni kwamba kugusa tupu kunachengua wudhuu´. Kujengea juu ya hilo ni kwamba mtu akigusa tupu yake wakati yuko anaoga basi ni lazima kutawadha baada ya hapo, ni mamoja amegusa kwa makusudi au pasi na kukusudia.
Maoni ya pili yanasema kuwa kugusa tupu hakuchengui wudhuu´; inapendeza tu kutawadha. Hilo ndio chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na ndio maoni yaliyo karibu na usahihi, khaswa pale ambapo mtu hakukusudia kuigusa. Hata hivyo salama zaidi ni mtu atawadhe.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/203)
- Imechapishwa: 10/05/2026
Swali: Mtu akigusa dhakari yake wakati wa kuoga josho la janaba. Je, unachenguka wudhuu´ wake?
Jibu: Maoni yanayotambulika katika madhehebu ni kwamba kugusa tupu kunachengua wudhuu´. Kujengea juu ya hilo ni kwamba mtu akigusa tupu yake wakati yuko anaoga basi ni lazima kutawadha baada ya hapo, ni mamoja amegusa kwa makusudi au pasi na kukusudia.
Maoni ya pili yanasema kuwa kugusa tupu hakuchengui wudhuu´; inapendeza tu kutawadha. Hilo ndio chaguo la Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na ndio maoni yaliyo karibu na usahihi, khaswa pale ambapo mtu hakukusudia kuigusa. Hata hivyo salama zaidi ni mtu atawadhe.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/203)
Imechapishwa: 10/05/2026
https://firqatunnajia.com/kugusa-tupu-wakati-wa-kuoga/