Kula na kunywa katika kipindi cha swawm inayopendeza

Swali: Ni ipi hukumu ya kula na kunywa katika funga ya kujitolea?

Jibu: Kula na kunywa kipindi cha swawm kunaiharibu swawm. Ikiwa ni swawm ya faradhi anapata dhambi. Na ikiwa ni swawm inayopendeza hapana vibaya akafungua, kwa sababu ni swawm inayopendeza. Matendo yote yanayopendeza inafaa kuyasitisha, isipokuwa Hajj na ´Umrah. Hajj na ´Umrah ni wajibu kuvikamilisha ingawa ni zenye kupendeza. Hata hivyo inachukiza kwa mtu kukatisha matendo yanayopendeza isipokuwa kukiwepo sababu sahihi.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/275)
  • Imechapishwa: 10/05/2026