Swali: Baadhi ya watunzi wa vitabu wanasema kuwa ´Aqiydah ya kusema kuwa Qur-aan imeumbwa ni kufuru ndogo. Je, maneno haya ni sahihi?

Jibu: Hapana. Ni ukafiri mkubwa na ulinzi unaombwa kwa Allaah. Maana yake ni kwamba Allaah hazungumzi. Maana yake ni kwamba Allaah ni bubu na hazungumzi. Allaah amewakosoa wale wanaoabudia masanamu:

وَاتَّخَذَ قَوْمُ مُوسَىٰ مِن بَعْدِهِ مِنْ حُلِيِّهِمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ ۚ أَلَمْ يَرَوْا أَنَّهُ لَا يُكَلِّمُهُمْ وَلَا يَهْدِيهِمْ سَبِيلًا ۘ اتَّخَذُوهُ وَكَانُوا ظَالِمِينَ

“Watu wa Muusa walijifanyia, baada ya kuondoka kwake katika mapambo yao, umbo la ndama. Je, hawakuona kuwa huyo [ndama] hawasemeshi na wala hawaongozi njia? Walimfanya [kuwa mungu] na wakawa madhalimu.”[1]

Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia baba yake:

يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا

“Ee baba yangu! Kwa nini unaabudu vile visivyosikia na visivyoona na visivyokufaa kitu chochote?”[2]

Ambaye hana sifa hawezi mungu kama mfano wa masanamu, mawe na vyenginevo. Ambaye hawezi kunufaisha na kudhuru hawezi kuwa mungu.

[1] 07:148

[2] 19:42

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 04/05/2023