Khatari ya Uislamu wa mtu asiyependa na kuchukia

Swali: Ni ipi hukumu ya kupinga jambo la kuchukia katika dini ya Allaah? Je, Uislamu wa mtu unasihi asipowachukia mayahudi na wakristo?

Jibu: Ni lazima kupenda na kuchukia. Kuwachukia maadui wa Allaah na kuwapenda mawalii wa Allaah. Mtu anatakiwa kuwachukia wao na dini yao. Hii ndio (البراء). Kuhusu kupenda (الولاء) maana yake mtu anatakiwa kumpenda Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwapenda waja wa Allaah ambao ni waumini. Mtu anatakiwa kuwapenda:

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ

“Hakika mna kigezo kizuri… ”

Bi maana kiigizo chema.

فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِهُ

“… kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: “Hakika sisi tumejitenga mbali nanyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah… ”

Alijtenga mbali nao na masanamu yao ambayo ndio waabudiwa wao:

كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ

”… tunakukanusheni na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha milele mpaka mtapomuamini Allaah pekee.” (60:04)

Haijuzu kuwapenda makafiri. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na manaswara marafiki – wao kwa wao ni marafiki – na yeyote atakayewafanya marafiki basi yeye ni katika wao. Hakika Allaah haongoi watu madhalimu.” (05:51)

Jambo lina khatari kubwa. Kupenda na kuchukia ni msingi miwili katika misingi ya dini hii. Dini haisihi isipokuwa kwa misingi miwili hiyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 04/05/2023