Kufurahi katika mnasaba wa kufanya tendo jema ni katika kujionyesha?

Swali: Mimi ni imamu wa msikiti na huwaongoza watu katika swalah ya Tarawiyh na wakati mwingine watu wananisifu kwa kusema “sauti yako ni nzuri” na mfano wa hayo na matokeo yake hufurahi kwa hilo. Je, hili ni katika kujionyesha?

Jibu: Hapana, sio katika kujionyesha. Ikiwa kwa kisomo chako hukukusudia sifa za watu, sio katika kujionyesha. Watu wakikusifu huna dhambi yoyote wewe kwa hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hii ni bishara njema kwa muumini.”

Pale watapokutaja kwa kheri na wewe hukukusudia kujionyesha au kutaka kusikika.