Mwanamke kujifunza Qur-aan kupitia vyombo vya khabari

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kusoma Qur-aan kwa njia ya kujifunza na sauti yake ikasikika kwenye redio au kwenye TV ili aweze kujifunza Qur-aan?

Jibu: Ajifunze Qur-aan kwa njia nyingine isiyokuwa hii. Ajifunze Qur-aan nyumbani kwake na kwenye masomo. Kuhusiana na kujifunza Qur-aan kupitia vyombo vya khabari mbele za watu na watu wakasikia, hili ni jambo halina asli. Sauti ya mwanamke ni ´Awrah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (80) ttp://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir_08_03_1433.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020