Kufunga Sha´baan inakuwa kamili au nusu yake?

Swali: Kufunga Sha´baan inakuwa kamili au nusu yake?

Jibu: Afunge siku zake nyingi au yote. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifunga siku zake nyingi au karibu yote isipokuwa siku chache.

Swali: Vipi maoni yanayosema kuwa mtu afunge siku kumi na tano za mwanzo kuanzia mwanzo wa Sha´baan?

Jibu: Hapana. Afunge siku zake nyingi au zote. Hii ndio Sunnah.

Swali: Je, inafaa kwake kuunganisha Sha´baan na Ramadhaan ikiwa ataanza Sha´baan kuanzia mwanzo wake au ale siku moja au siku mbili kati ya hizo mbili?

Jibu: Akila kati ya Sha´baan an Ramadhaan ndio bora zaidi. Vinginevyo inafaa kwake. Umm Salamah amesema:

“Alikuwa akiifunga [Sha´baan] yote.”

Katika upokezi mwingine kutoka kwa ´Aaishah:

“Alikuwa akiifunga [Sha´baan] yote.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22355/هل-السنة-صوم-شعبان-كله-او-بعضه
  • Imechapishwa: 24/02/2023