Swali: Ni ipi hukumu ya swawm ya ambaye hakula daku?

Jibu: Hapana vibaya. Funga yake ni sahihi. Lakini ameacha Sunnah. Sunnah ni yeye kula daku. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuleni daku. Kwani hakika katika daku kuna baraka.”

Daku ni Sunnah; ni mamoja swawm ni ya faradhi au imependekezwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akila daku. Sunnah ni yeye kula daku kwa kile kilichomkuia chepesi kama vile tende, chakula au tunda. Kitu hicho kinamsaidia katika funga yake. Akifunga bila kula daku hapana neno na swawm yake ni sahihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baadhi ya Maswahabah zake waliwahi kufunga siku mbili mfululizo pasi na kula daku wala kukata swawm.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.binbaz.org.sa/mat/18661
  • Imechapishwa: 18/04/2022