Ni vipi mtatangamana na wafanya kazi na majirani wenu wakristo? Mnatakiwa kutaamiliana nao kama wao wanavyotaamiliana nanyi. Kwani hakika kufanya hivo ni katika kufanya uadilifu ambao Allaah (Ta´ala) ameamrisha. Hakika Allaah (Ta´ala) amesema:
إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ
“Hakika Allaah anaamrishia uadilifu na wemaa na kuwapa [mahitajio na msaada] jamaa wa karibu.”[1]
Hapana vibaya kuwatendea wema kwa ajili ya kuwapenzea kuingia katika Uislamu, lakini sio kwa ajili ya kuwapenda au kwa ajili ya kujikombakomba kwao. Allaah (Ta´ala) amesema:
لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ
”Allaah hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika dini na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu – hakika Allaah anapenda wafanyao uadilifu.”[2]
Hata hivyo haifai kwetu kuwapenda kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:
لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ
“Hutopata watu wanaomuamini Allaah na siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wale wanaopinzana na Allaah na Mtume Wake, japo wakiwa ni baba zao, watoto wao, ndugu zao au jamaa zao.”[3]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ
“Enyi mlioamini! Msimchukue adui Wangu na adui wenu kuwa marafiki mkiwapelekea mapenzi na hali wamekwishakanusha haki iliyokujieni.”[4]
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ َ
“Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na manaswara marafiki.”[5]
Kuhusu kuwapongeza, hapana shaka yoyote kwamba ni haramu ikiwa inahusiana na minasaba ya kidini. Kwa sababu kuwapongeza maana yake mtu anaridhia ukafiri wao, kutia moyo na kuwashaji´isha. Ikiwa mapongezi yanahusiana na minasaba mingine isiyokuwa ya kidini kama vile kupata pesa, kupata mtoto mchanga na mfano wake, hapana vibaya kuwapongeza ikiwa wao watatupongeza ili tuwe waadilifu na tufanye inswafu. Vinginevyo hatutowapongeza isipokuwa ikiwa kuacha kuwapongeza kutapelekea sisi kudhurika. Kuhusu kuwapa rambirambi; tutawapa pole ya kufiwa ikiwa wao wanatupa pole ya kufiwa kwa ajili ya kufanya uadilifu na inswafu. Hata hivyo kuwapa kwetu pole ya kufiwa inapaswa iwe njia fulani ya kuwapa mawaidha na kuwalingania katika Uislamu.
[1] 16:90
[2] 60:8
[3] 58:22
[4] 60:1
[5] 5:51
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/381-382)
- Imechapishwa: 22/06/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/381-382)
Imechapishwa: 22/06/2026
https://firqatunnajia.com/kufanya-uadilifu-bila-ya-mapenzi/