Kukusanyika watu nyumbani kwa mfiwa kwa lengo la kutoa rambirambi na kukodisha msomaji wa Qur-aan asome Qur-aan ni Bid´ah kutokana na sababu zifuatazo:
1 – Matendo hayo hayakuwa yenye kutambulika kipindi cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Ni jambo linalotambulika kwamba kutoa rambirambi ni katika Bid´ah, na ikiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah zake hawakukusanyika katika mikusanyiko hiyo, basi ina maana kwamba ni Bid´ah. Msingi wa ´ibaadah ni kukomeka isipokuwa yale yanayofahamishwa na dalili. Ikishathibiti kuwa ni Bid´ah, basi imethibiti vilevile kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametahadharisha kutokana na Bid´ah na kwamba kila Bid´ah ni upotofu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ninakutahadharisheni na mambo yaliyozuliwa, kwani hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[1]
Maneno yake ni ya aina ya ueneaji wenye nguvu kabisa, yanayotoka kwa mtu ambaye ndiye mjuzi zaidi wa Shari´ah ya Allaah na mafahmisho ya maneno yake. Kwani hakika yeye ndiye kiumbe ambaye alikuwa mwenye kuwatakia watu mema zaidi na mwenye ufaswaha zaidi kubainisha. Hakuna muumini yeyote anayetilia shaka jambo hilo. Hakujatoka herufi hata moja kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inayobagua kanuni hii yenye kuenea. Kuhusiana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:
“Yeyote mwenye kuweka katika Uislamu njia nzuri basi atapewa ujira kwayo na ujira wa yule mwenye kuifanya mpaka siku ya Qiyaamah.”[2],
makusudio sio kwamba azushe ndani ya Shari´ah ya Allaah yasiyokuwemo kabisa. Kwani makusudio yangelikuwa hayo basi yangelikuwa yanapingana na maneno yake yaliyokwishatangulia:
“Ninakutahadharisheni na mambo yaliyozuliwa, kwani hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”
Jengine ni kwamba dini ya ummah ingelikuwa yenye kutofautiana ambapo kila kundi likifurahikia mrengo wao. Matokeo yake ummah ungelipatwa na maneno Yake (Ta´ala):
إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ ۚ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّـهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ
“Hakika wale waliofarikisha dini yao na wakawa makundi makundi huna lolote kuhusiana na wao. Hakika amri yao iko kwa Allaah, kisha atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakifanya.”[3]
Makusudio ya “Yeyote mwenye kuweka katika Uislamu njia nzuri” hapana vyengine isipokuwa inaweza kufasiriwa kwa njia mbili:
1 – Ambaye ameharakia kufanya kitendo ambacho kimeshathibiti ndani ya dini. Tafsiri hiyo inafahamishwa na sababu ya Hadiyth. Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Tulikuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanzoni mwa mchana wakati walipokuja watu waliokuwa uchi. Nguo zao zilikuwa za kuchanika na panga zao zilikuwa zimenolewa. Wengi wao walikuwa ni kutoka Mudhwar. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoona ufakiri walionao sura yake ikabadilika. Akaingia kisha akatoka. Halafu akamwamrisha Bilaal aite kwa ajili ya swalah. Wakaswali na kuhubiri na kusoma:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا
“Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja na akaumba kutoka humo mke wake na akaeneza kutoka hao wawili wanaume wengi na wanawake na mcheni Allaah ambaye Kwake mnaombana na jamaa. Hakika Allaah amekuwa juu yenu Mwenye kuchunga.”[4]
na:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ
“Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na nafsi itazame imetanguliza nini kwa ajili ya kesho na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mjuzi kwa myatendayo.”[5]
Mtu anaweza kutoa swadaqah ya dinari, dirhamu, nguo, ngano hata kipande cha tende.” Mtu mmoja kutoka Answaar akaja na mfuko ambao ulikaribia kumshinda kuubeba. Watu wakaanza kuleta baada yake mpaka nikaona matuta mawili ya chakula na nguo. Uso wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ukanawiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“ Yeyote mwenye kuweka katika Uislamu njia nzuri basi atapewa ujira kwayo na ujira wa yule mwenye kuifanya mpaka siku ya Qiyaamah. Na yeyote mwenye kuweka katika Uislamu njia mbaya ataadhibiwa kwao na adhabu ya yule atakayeufanya pasi na kupunguziwa chochote katika adhabu zao.”[6]
2 – Ambaye atahuisha njia iliowekwa katika Shari´ah baada ya kuachwa kwake. Miongoni mwa hayo ni yale maneno yake ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) baada ya kuwaamrisha watu kuswali kisimamo cha Ramadhaan nyuma ya imamu mmoja:
“Ni uzuri wa Bid´ah uliyoje.”
Kwa maana hiyo Haiyth itakuwa imekusudia ambaye atahuisha njia nzuri baada ya kuachwa kwake.
Wanazuoni wengi wamezungumzia hukumu ya kukusanyika kwa ajili ya kutoa rambirambi. Katika “al-Muntahaa”, ambacho ni miongoni mwa vyanzo vya Hanaabilah waliokuja nyuma, imekuja ifuatavyo:
“Vikao vya kama hivyo vinachukiza.”
Imekuja katika maelezo:
“Kwa maana ya kwamba inachukiza kwa aliyepatwa na msiba kukaa maeneo fulani kwa ajili ya kupokea rambirambi.”
Imekuja katika “al-Muqniy´”:
“Inachukiza kukaa kwa ajili yake.”
Kwa ajili ya kutoa rambirambi. Imekuja katika “Sharh al-Kabiyr”:
“Limetajwa na Abul-Khattwaab na akasema kuwa kitendo hicho kimezuliwa.”
an-Nawawiy amesema katika “al-Majmuu´”:
“Kuhusu kukaa kwa ajili ya kutoa mkono wa pole, ash-Shaafi´iy, mtunzi na maswahiba wengine wamesema kuwa kitendo hicho kinachikiza.”
Akasema baada ya hapo:
“Mtunzi na wengineo wakajengea hoja yao kwa dalili nyingine, nayo ni kwamba kitendo hicho kimezuliwa.”
al-Albaaniy amesema:
“Inatakikana kuepuka mambo mawili ingawa watu wamezowea kuyafanya:
1 – Kukusanyika kwa ajili ya kutoa rambirambi maeneo fulani kama vile kwenye nyumba, makaburini au msikitini.
2 – Wafiwa kuwapikia chakula wale wanaokuja kutoa mkono wa pole. Kwa sababu Jariyr bin ´Abdillaah al-Bajaliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Tulikuwa tukizingatia kukusanyika kwa familia ya maiti na kutengeneza chakula baada ya mazishi ni aina fulani ya kuomboleza.”[7][8]
Katika kitabu hichohicho al-Albaaniy amemnukuu al-Hammaam ambaye amesema kuwa kitendo hicho ni Bid´ah mbaya. Kuhusu ambaye atayasapoti matendo haya kwamba eti ni mazuri, yanarudishwa nyuma na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“… na kila Bid´ah ni upotofu.”
Baadhi wanajengea hoja kuwa eti yapo mambo mengi hii leo yanayofanywa ambayo hayakuwepo katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ambayo hayazingatiwi kuwa ni Bid´ah. Jawabu ni kwamba ikiwa mambo mepya hayo yanafanywa kwa lengo la ´ibaadah na kujikurubisha kwa Allaah basi ni Bid´ah na upotofu. Ikiwa ni njia inayopelekea katika jambo lililowekwa katika Shari´ah, kama vile kuzigawanya elimu na kuchapisha vitabu, basi nayo yamewekwa katika Shari´ah.
Kuhusu kuleta msomaji anayesoma Qur-aan kwa ajili ya kutoa rambirambi, ikiwa ni kwa kupokea malipo basi hapati thawabu zozote na isitoshe anapaha dhambi. Kwa msemo mwingine maiti hanufaiki kwa kisomo chake. Na ikiwa msomaji anasoma pasi na kupokea malipo, basi kusoma kwa ajili ya rambirambi ni Bid´ah na mtu halipwi thawabu kwa jambo hilo. Ni wajibu kwa muumini kurejea katika yale waliyokuwemo Salaf, kwa sababu wao ndio karne bora. Yale ambayo watu wamezua ndani ya dini ya Allaah (Ta´ala) yanapaswa kupuuzwa, ni mamoja katika jambo hili na mengineyo. Kheri zote zinapatikana katika kuwafuata wale waliotangulia, na shari zote zinapatikana katika kuzua wale waliokuja nyuma. Allaah atuwafikishe sisi wote katika kufuata Sunnah na kujiepusha na Bid´ah. Ni wajibu kwa wanazuoni kubainisha haki katika jambo hili na mengineyo kwa mujibu wa vile alivyotaja Allaah (Ta´ala):
ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ
“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.”[9]
Haijuzu kwao kwenda katika mikusanyiko kama hii kwa ajili ya ramrambi isipokuwa ikiwa ni kwa lengo la kutoa nasaha.
[1] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (34). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2455).
[2] Muslim (1017).
[3] 6:159
[4] 4:1
[5] 59:18
[6] Swahiyh.
[7] Ahmad (2/204) na Ibn Maajah (1612).
[8] Ahkaam-ul-Janaa-iz.
[9] 16:125
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/377-380)
- Imechapishwa: 22/06/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/377-380)
Imechapishwa: 22/06/2026
https://firqatunnajia.com/mikusanyiko-ya-kutoa-rambirambi-na-kukodisha-msomaji-wa-qur-aan/