Swali: Ni ipi Radd kwa mwenye kukhusisha kufanya tendo jema siku ya maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na aliyopokea Imaam Muslim katika “as-Swahiyh” yake wakati alipoulizwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwa nini anafunga siku ya Jumatatu ambapo akasema:
“Hiyo ni siku niliyozaliwa.”?
Jibu: Ndio, kufunga ni sawa. Ama kuzusha tendo lisilokuwa swawm katika siku hii, hapana. Isitoshe, ni nani anaweza kuweka kikomo siku ambayo alizaliwa Mtume? Hakukuthibiti siku maalum. Hakubainisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni siku ipi [tarehe] aliyozaliwa katika mwaka. Lililowekwa katika Shari´ah ni kufunga tu. Ama kusherehekea [kuzaliwa kwake] na mambo mengine ni Bid´ah.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-8.mp3
- Imechapishwa: 20/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)