Kufaa kusoma vitabu vya tafsiri ya Qur-aan bila twahara

Swali: Je, inafaa kugusa tafsiri ya Qur-aan pasi na kuwa na twahara?

Jibu: Inafaa kuhusa vitabu vya tafsiri pasi na kizuizi wala twahara. Vitabu hivyo haviitwi kuwa “msahafu”. Kuhusu msahafu ambao ndani mna Qur-aan peke yake haijuzu kuugusa kwa asiyekuwa na twahara. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ

“Hakika hii ni Qur-aan tukufu. Katika Kitabu kilichohifadhiwa. Haigusi isipokuwa waliotakaswa kabisa.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiiguse Qur-aan isipokuwa aliye na twahara.”

Msingi wa twahara yenye kuachiwa katika istilahi ya Shari´ah ni pale mtu anapokuwa msafi kutokamana na hadathi ndogo na kubwa. Isitoshe hivo pia ndivo walivofahamu Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kutokana na tunavojua haikuhifadhi kutoka kwa yeyote miongoni mwao kwamba aligusa msahafu pasi na twahara. Haya ndio maoni ya jopo kubwa la wanazuoni, na ndio maoni ya sawa.

[1] 56:77-79

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/148)
  • Imechapishwa: 24/08/2021