Kufaa kumwombea du´aa mbaya aliyekudhulumu

Swali: Kitendo cha Sa´d kumwombea du´aa mbaya aliyemdhulumu kinafahamisha kuwa inafaa kufanya hivo?

Jibu: Ndio. Ni kama alivosema Allaah (´Azza wa Jall):

لَّا يُحِبُّ اللَّـهُ الْجَهْرَ بِالسُّوءِ مِنَ الْقَوْلِ إِلَّا مَن ظُلِمَ

“Allaah hapendi uovu utajwe hadharani isipokuwa kwa yule ambaye kadhulumiwa.”[1]

Inafaa kwa aliyedhulumiwa kumwombea du´aa mbaya aliyemdhulumu ijapo ni kwa sauti ya juu.

[1] 04:148

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23170/ما-حكم-الدعاء-على-الظالم
  • Imechapishwa: 18/11/2023