Kubusu kichwa cha mzazi, mwanachuoni na mzee

Swali: Je, inafaa kubusu kichwa cha mzazi, mwanachuoni au mtumzima? Je, kumepokelewa Hadiyth juu ya hilo?

Jibu: Hakuna neno kubusu kichwa cha mtumzima, mzazi wa kiume au mzazi wa kike. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimbusa kichwa Faatwimah wakati anapoingia. Anasimama kwa ajili yake na kumbusu na yeye Faatwimah anasimama kwa ajili yake na kumbusu. Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) alipofika baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuaga dunia alikuwa amefunikwa ambapo akamfunua uso wake na kumbusu kati ya macho yake na kusema:

“Namtoa fidia baba na mama yangu. Ulikuwa mzuri ulipokuwa hai na baada ya kufa.”

Hapana neno akimbusu Mahram yake, mwanaume kwa mwanaume mwenzake, mwanamke kwa mwanamke mwenzake au Mahram akambusu mama au dada yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23167/حكم-تقبيل-جبهة-الوالد-والعالم-والكبير
  • Imechapishwa: 18/11/2023