Swali: Ni ipi hukumu ya kuuza baada ya adhaana misikitini?
Jibu: Haijuzu kuuza baada ya adhaana ya pili ya ijumaa pale Khatwiyb anapoingia. Kuhusu swalah nyinginezo bora ni kutofanya hivo, kwa sababu hakukupokelewa chochote juu ya hilo. Adhaana ikishatolewa basi mtu afanye haraka kwenda katika swalah na asishughulishwe na kuuza wala kitu kingine chochote baada ya adhaana. Hata hivyo dalili imetajwa kuhusu swalah ya ijumaa kutokana na ufinyu wa wakati wake na ukubwa wa jambo lake. Aidha madhumuni ya swalah ni kuhudhuria Khutbah. Kwa hivyo ikiwa atajishughulisha na jambo atakosa Khutbah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25127/حكم-البيع-بعد-الاذان-عند-المساجد
- Imechapishwa: 05/02/2025
Swali: Ni ipi hukumu ya kuuza baada ya adhaana misikitini?
Jibu: Haijuzu kuuza baada ya adhaana ya pili ya ijumaa pale Khatwiyb anapoingia. Kuhusu swalah nyinginezo bora ni kutofanya hivo, kwa sababu hakukupokelewa chochote juu ya hilo. Adhaana ikishatolewa basi mtu afanye haraka kwenda katika swalah na asishughulishwe na kuuza wala kitu kingine chochote baada ya adhaana. Hata hivyo dalili imetajwa kuhusu swalah ya ijumaa kutokana na ufinyu wa wakati wake na ukubwa wa jambo lake. Aidha madhumuni ya swalah ni kuhudhuria Khutbah. Kwa hivyo ikiwa atajishughulisha na jambo atakosa Khutbah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25127/حكم-البيع-بعد-الاذان-عند-المساجد
Imechapishwa: 05/02/2025
https://firqatunnajia.com/kuendelea-na-biashara-baada-ya-adhaana/