Swali: Umetaja masharti na sunnah za kuchinja na hukutaja kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja. Ni ipi hukumu?

Jibu: Kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja sio wajibu[1]. Mtu anaweza kuchinja kichinjwa chake ijapokuwa hakuelekea Qiblah. Lakini wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema kuwa bora zaidi ni mtu aelekee Qiblah. Kwa sababu ni ´ibaadah. Lakini hata hivyo hawakusema kuwa ni sharti. Iwapo mtu atachinja kwa kuelekea upande usiokuwa Qiblah ni halali. Sio jambo limechukizwa. Hapana neno. Tofauti na wanavosema watu wasiokuwa na elimu. Baadhi yao wanasema kwamba ni lazima kuelekea Qiblah, jambo ambalo si sahihi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kutoelekea-qiblah-wakati-wa-kuchinja-na-kusema-bismillaah/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/978
  • Imechapishwa: 20/12/2018