Swali: Vipi kuelekea Qiblah safarini?

Jibu: Akiwa safarini anaruhusiwa kuswali juu ya kipando katika swalah inayopendeza na swalah ya faradhi pale atapohitajia. Ama swalah inayopendeza ataswali safarini na akiwa mjini. Hata hivyo haifai ikiwa ni swalah ya faradhi; anatakiwa kusimama na kuelekea Qiblah. Isipokuwa kama kuna dharurah kwa mfano wa mafuriko makubwa na mvua inayonyesha. Katika hali hiyo itafaa kwake kuswali juu ya kipando na ataelekea Qiblah kwa kuashiria, kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Ni lazima kuelekea Qiblah?

Jibu: Ni lazima katika swalah ya faradhi. Lakini ikiwa ni swalah inayopendeza ataswali kule kilipoelekea kipando chake. Anaposwali swalah inayopendeza juu ya kipando chake ataswali kule kilipoelekea kipando chake. Akianza swalah yake kwa kuelekea Qiblah kisha baadaye akaelekea kule kilipoelekea kipando chake ndio bora zaidi. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaposwali swalah inayopendeza anaelekea Qiblah kisha anaelekea upande wa safari yake.”

Hivi ndio bora zaidi. Ni sawa pia akiswali kule kinapoelekea kipando chake licha ya kwamba ni mwanzo wa safari yake, kama alivyosimulia ´Aamir bin Rabiy´ah, Anas na wengineo. Wamesimulia kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa safarini anaelekea upande wa safari yake. Akikusudia katika swalah zinazopendeza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23115/حكم-استقبال-القبلة-في-الصلاة-في-السفر
  • Imechapishwa: 06/11/2023