Swali: Ni wavukaji mipaka wepi waliokusudiwa katika Aayah:

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ

“Muombeni Mola wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye hawapendi wenye kuvuka mipaka.”[1]?

Jibu: Ni wale wenye kuomba jambo lenye madhambi na kukata kizazi. Baadhi ya Salaf wamesema:

“Ni kule mtu kunyanyua juu sauti pasipo haja.”

Hata hivyo ukweli wa mambo kuchupa mipaka ni kwa yule anayeomba jambo lenye madhambi. Kwa mfano mtu amwombe Allaah amsaidie aweze kuzini au kuiba. Huku ni kuchupa mipaka. Au awaombee watu du´aa mbaya pasi na haki. Hii ni dhambi. Au akawaombea jamaa zake du´aa mbaya pasi na haki. Huku ni kukata kizazi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna mja yeyote anayemuomba Allaah wala kukata kizazi isipokuwa Allaah humpa moja kati ya mambo matatu… “

Bora na salama zaidi ni kuacha kuomba kwa kupaza juu sauti, kwa sababu baadhi ya Salaf walikuwa wanaona kufanya hivo ni kuchupa mipaka katika du´aa akipaza juu sauti yake. Lakini akiwa ni imamu atanyanyua sauti yake, mfano wa Qunuut ya Witr, Qunuut ya majanga na katika Khutbah na ili wasikilizaji waitikie “Aamiyn”. Lakini mtu akiomba du´aa peke yake katika Sujuud, mwishoni mwa swalah au maeneo mengine inapendeza na ni bora kuomba kimyakimya. Amesema (Ta´ala):

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً

“Muombeni Mola wenu kwa unyenyekevu na kwa siri.”[2]

[1] 07:55

[2] 07:55

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23117/ما-معنى-الاعتداء-في-انه-لا-يحب-المعتدين
  • Imechapishwa: 06/11/2023