71. Watoza zakaah wa Mtume walikuwa wanaitwa nani?

Swali 71: Watoza zakaah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wanaitwa nani?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimtuma al-Muhaajir bin Abiy Umayyah kwenda Swanaa’ ambapo al-Aswad al-‘Ansiy wakamshambulia yeye na Banuu Asad pia.

Alimtuma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Maalik bin Nuwayrah kuchukua zakaah kutoka kwa Banuu Handhwalah, kisha zakaah za Banuu Sa’d zikagawanywa kwa az-Zarbaqaan bin Badr na Qays bin ´Aaswim.

al-‘Alaa’ bin al-Hadhwramiy alitumwa kwenda Bahrain.

Aliy bin Abiy Twaalib alitumwa kwenda Najran, kukusanya zakaah na kodi za kulindwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 143
  • Imechapishwa: 06/11/2023