Kudai haki yako katika mahakama ya kisekula

Swali: Nina biashara nje ya nchi na nimetapeliwa huko. Je, inafaa kwangu kutafuta haki yangu katika mahakama inayohukumu kinyume na Shari´ah ili niweze kupata haki yangu?

Jibu: Ikiwa unataka kuhakikisha kupata haki yako tu na wala hutomdhulumu yeyote, inafaa. Wewe lengo lako ni kupata haki yako na si kumdhulumu yeyote. Hapana vibaya. Hata hivyo haijuzu ikiwa unataka kuhukumiana kwa sheria zilizotunga wanadamu kwa lengo la kuchukua haki za watu au kutumia fursa ya kanuni hizo kwa ajili ya kikiuka haki za watu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 21/05/2023