Kuchelewesha zakaah kwa ajili ya kwenda nchi nyingine

Swali: Sijatoa zakaah ya mwaka mzima uliyopita kwa sababu ya nataka nisafiri na kuwapa nayo mafukara huko. Je, inafaa kwangu kufanya hivo?

Jibu: Ndio, inafaa kuchelewesha zakaah kwa lengo sahihi. Ikiwa huko unakokwenda kuna mafukara ambao wanahitaji zaidi kuliko wengine, basi kitendo hicho hakina neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 21/05/2023