Swali: Ni ipi hukumu ya dini juu ya mtu kubadilisha uraia wake, sawa ubadilishaji huu ikiwa ni kutoka katika mji wa kiarabu wa Kiislamu na kwenda katika mji wa kiarabu wa Kiislamu mwingine, kutoka katika mji wa kiarabu wa Kiislamu na kwenda katika mji wa kiulaya pamoja na mtu kushikamana na ´Aqiydah yake ya Kiislamu?

Jibu: Muislamu kuhamisha uraia wake kutoka katika nchi ya Kiislamu na kwenda uraia wa nchi nyingine ya Kiislamu inajuzu. Ama muislamu kuhamisha uraia wake kutoka katika nchi ya Kiislamu na kwenda katika uraia wa nchi ya kikafiri haijuzu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/72)
  • Imechapishwa: 24/08/2020