Kafiri kuchukua uraia wa nchi ya Kiislamu

Swali: Ni ipi hukumu ya kafiri kuchukua uraia wa nchi ya Kiislamu?

Jibu: Kafiri kuchukua uraia wa nchi ya Kiislamu inajuzu midhali kunaaminika fitina juu yake na kunatarajiwa kheri juu yake. Lakini hata hivyo asiachwe akaishi katika kisiwa cha waarabu isipokuwa akiingia katika Uislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameusia kuwatoa washirikina katika kisiwa cha waarabu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/74)
  • Imechapishwa: 24/08/2020