Inafaa kufanya kazi katika mji wa kikafiri?

Swali: Je, muislamu kufanya kazi katika nchi ya kikafiri inajuzu? Je, kitendo cha Yuusuf kinaingia katika hili?

Jibu: Ikiwa anajiamini fitina juu ya nafsi yake katika dini yake na akawa ni mwenye kujihifadhi na ni mjuzi akitarajia kuwatengeneza wengine na manufaa yake yakawa yataenea kwa wengine na asiwasaidie katika batili, itakuwa inajuzu kufanya kazi katika nchi ya kikafiri. Miongoni mwa watu hawa kunaingia pia Yuusuf (´alayhis-Swalaatu was-Salaam). La sivyo itakuwa haijuzu.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/275)
  • Imechapishwa: 24/08/2020