Jinsi ya kutangamana na jirani mnaswara na sikukuu zake

Swali: Vipi mtu atataamiliana na mnaswara jirani wa nyumba yangu au masomo? Je, nimtembelee na kumpa hongera kwa sikukuu yake?

Jibu: Inajuzu kutangamana na mnaswara jirani kwa kumfanyia ihsani, kumsaidia katika mambo yanayoruhusu, kumtendea wema na kumtembelea ili kumlingania katika dini ya Allaah (Ta´ala) pengine Allaah akamwongoza katika Uislamu.

Kuhusu kuhudhuria sikukuu zao na kuwapongeza kwazo haijuzu kufanya hivo. Amesema (Subhaanah):

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖوَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Shirikianeni katika wema na kumcha Allaah na wala msishirikiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Kuhudhuria sikukuu zao na kuwapongeza kwazo ni aina moja wapo ya kuwapenda ambako kumeharamishwa. Hali kadhalika kuwafanya marafiki.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/67-68)
  • Imechapishwa: 24/08/2020