Swali: Je, inajuzu kuishi kwa mshirikina mwenye makuba na mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah?

Jibu: Haijuzu kuishi kwa mshirikina miongoni mwa watu wa makuba na anayechinja kwa ajili ya siyekuwa Allaah. Anaweza kumuathiri na kumuita katika shirki zake. Isipokuwa tu ikiwa kama atakuwa ametenzwa nguvu kufanya hivo au akaona kuna maslahi kwa kufanya hivyo ili kumlingania katika dini ya Allaah na kumwelekeza ajihadhari. Pengine kwa kufanya hivo Allaah akamwongoza na kumuelekeza katika kukubali haki.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/63-64)
  • Imechapishwa: 24/08/2020