Swali: Ni ipi hukumu ya kuchelewesha zakaah ya dhahabu mwezi mmoja au miwili?

Jibu: Ikiwa ni kwa haja ni sawa. Mfano wa haja kama hiyo ni kama pesa ziko mbali au hana pesa kwa sasa. Haina neno. Lakini aandike uchelewaji. Ni deni alonalo la Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf%2030-7-1434_01.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2020