Kuchelewesha Tarawiyh mpaka mwishoni mwa usiku

Swali: Je, inafaa kuchelewesha swalah ya Tarawiyh mpaka mwisho wa usiku?

Jibu: Ndio, ni sawa. Ikisahilika kufanya hivo mwishoni mwa usiku ndio bora. Ikiwepesika kufanya hivo mwishoni mwa usiku ndio bora. Waislamu wanaswali mwanzoni mwa usiku kwa sababu ndio kunawapa uchangamfu zaidi na kuko karibu zaidi kuitekeleza. Kwa sababu watu wengi wakilala watashindwa kuamka mwishoni mwa usiku. Kwa hivyo ikiwepesika kuiswali mwishoni mwa usiku ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18500/تاخير-صلاة-التراويح-الى-اخر-الليل
  • Imechapishwa: 10/04/2023