Je, niswali Witr baada ya adhaana ya kwanza ya Fajr?

Swali: Je, niswali Witr baada ya adhaana ya kwanza?

Jibu: Witr ni katika usiku wote. Kuanzia baada ya swalah ya ´Ishaa mpaka kuchomoza kwa alfajiri. Usiku wote ni wakati wa kuswali Witr. Baada ya kumaliza swalah ya ´Ishaa na Sunnah zake za Raatibah mpaka kuchomoza kwa alfajiri. Wakati wote huu ni wa Witr. Ikiwepesika mwishoni mwa usiku ndio bora. Vinginevyo swali Witr kabla ya kulala. Ukiogopa kutoweza kuamka basi bora ni kuswali Witr kabla ya kwenda kulala.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18874/هل-يجوز-صلاة-الوتر-بعد-الاذان-الاول
  • Imechapishwa: 10/04/2023